Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph
Konyo.
Watu watano wamefariki dunia papo hapo katika kijiji cha Shilabela, kata ya
Bwanga, wilayani Chato, mkoa wa Geita, baada ya kupigwa na radi wakati
wakiendelea na ibada ya Sikukuu ya Pasaka.
Tukio hilo lilitokea juzi jioni kwenye Kanisa la Assemblies of God Tanzania (AGT) na kujeruhi watu wengine 18 wakati wakiwa kwenye maadhimisho ya sikukuu ya kufufuka kwa Yesu Kristo, Pasaka. Kati ya majeruhi hao, wanne wamelazwa katika Zahanati ya Bwanga, wilayani Chato.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo, akizungumza na NIPASHE jana, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliofariki ni Daud Merdad (20), Daud Lazaro (20), Saimon Marco (15), Haile Shija (20) na Monica Sumuni (19).

No comments:
Post a Comment