Idara ya Uhamiaji yafukuza raia wa kigeni 1,796

Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Abbass Irovya akitoa taarifa yake mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
2
Kutoka kushoto ni Mratibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji, Rosemary Mkandala, Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Abbass Irovya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Wilson Bambaganya na Ofisa Habari, Leslie Mbotta.
3.Wanahabari wakichukua tukio hilo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
IDARA ya Uhamiaji leo imeeleza juu ya mpango mkakati wa kuhakikisha inapambana na kuwachukulia hatua kali za kisheria dhidi yao wahamiaji haramu wa kigeni wanaoingia nchini bila vibali maalum ambapo pia imeleza operesheni ondoa uhamiaji haramu iliyoanza tangu Desemba mwaka jana na kuwakamata raia wa kigeni takribani 4,792 kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu za uhamiaji katika kipindi cha January hadi aprili mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Abbass Irovya amesema operesheni hiyo imefanikiwa kuwafukuza raia 1,796 wa kigeni kwa kukiuka sheria za uhamiaji na kuongeza kuwa waliohukumiwa kifungo ni 132 na 383 kesi zao zipo mahakamani zinaendelea katika mikoa mbalimbali hapa nchini na raia 294 waliachiwa huru baada ya kugundulika hawana hatia.
Aidha, Irovya aliwapongeza wananchi kwa kutoa ushirikiano katika Idara ya Uhamiaji kufanikisha kuwakamata wahamiaji haramu kutokana na uelewa mpango mkakati wa kutoa elimu juu yao ambayo imepelekea kupata mafanikio makubwa.

No comments:

Post a Comment