CHENGE, CHENGE, CHENGE TENA?


Makala: Ojuku Abraham

KAMA Mwalimu Julius Kambarage Nyerere angekuwa bado anatawala nchi hii, ni watu wachache sana wangeweza kulijua jina la Andrew Chenge, yule mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, aliyekaa katika ofisi hiyo kubwa na yenye heshima, kuanzia mwaka 1993 hadi 2005.
Lakini katika nchi ambayo inaendeshwa kwa hila na dili, jina hili linajipatia umaarufu na kuenziwa, bila kujali ni kwa kiasi gani, Watanzania zaidi ya milioni 45 wanaishi kwa dhiki na mateso kutokana na yeye kuitumia vibaya ofisi ya umma kujinufaisha.
Ni katika kipindi chake akiwa mwanasheria mkuu wa serikali, ndipo nchi yetu imeshuhudia kashfa za mikataba mingi mibovu, isiyo na tija kwa nchi, ikisainiwa.…

No comments:

Post a Comment