KWA NINI WATU WENGI HAWAFANIKIWI MAISHANI?



NI matumaini yangu kwamba msomaji wangu unaendelea vizuri na kazi ya kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo kupitia ujasiriamali. Mada tunayoendelea kuijadili ni sababu zinazofanya watu wengi washindwe kufanikiwa.
Wiki iliyopita, niliishia kueleza kwamba watu wengi hawafanikiwi kwa sababu hawawezi kuwa mabahili katika matumizi ya pesa wanazozipata. Niliishia kukupa mfano wa jinsi mimi na dada yangu tulivyokuwa na hulka tofauti za matumizi ya pesa tulipokwenda kwenye mashindano ya Umiseta mjini Songea.

Kabla sijaendelea mbele, ningependa kumalizia mfano huo:
Mzee wetu alitupatia Sh. 5,000 kila mtu kama ‘pocket money’ na pesa ya kutumia njiani wakati wa safari. Kwa wakati huo ilikuwa ni pesa nyingi sana kwa mwanafunzi. Pengine kwa nyakati hizi ingekuwa ni zaidi ya shilingi laki…

No comments:

Post a Comment