Ufafanuzi wa sababu za kusitishwa huduma umeeleza kuwa kichwa kimojawapo ambacho hutoa huduma kimepelekwa Karakana Kuu ya Morogoro kwa ajili ya ukarabati maalum na kwamba kinatarajiwa kurejeshwa Dar es Salaam jioni ya siku ya Jumapili.Novemba 16, 2014 baada ya kukamilika zoezi hilo la ukarabati.
Huduma zitarejea tena siku ya Jumatatu saa 12:30 asubuhi kuanzia kama kawaida kituo cha Ubungo Maziwa.
Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake! Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza!
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu. Dar es Salaam,Novemba 13, 2014
No comments:
Post a Comment