Rombo yaongoza kwenye pombe za kienyeji; Viwanda 21 vyafungiwa



Halmashauri ya wilaya ya Rombo imevifunga viwanda 21 vinavyotengeneza pombe haramu inayodaiwa kupunguza nguvu za kiume.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Elinasi Pallangyo aliyasema hayo juzi katika baraza la madiwani.

Alisema viwanda hivyo vilikuwa vikisababisha baadhi ya watu kujihusisha na unywaji wa pombe katika saa za kazi.

Alisema kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Wilaya imekuwa ikipambana na tatizo la pombe haramu, lakini uzalishaji huo ulikuwa ukiendelea. Alisema Rombo imekuwa ikiongoza kwa kutengeneza pombe za kienyeji zisizo na viwango.

“Halmashauri imeamua kufunga viwanda 21 vinavyozalisha pombe hizo zinazoharibu afya za vijana, kupunguza uzazi katika Wilaya hii na kukosa wanafunzi kutokana na uzazi kupungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Pallangyo.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mohamed Maja alisema wameziomba taasisi za dini kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na madhara ya pombe hizo. Alisema kikosi kazi kilichoundwa na mkuu wa wilaya kitasimamia idara ya biashara na kwamba mfanyabishara atakayekiuka agizo na kuuza pombe saa za kazi atatozwa faini
http://www.wavuti.com/



No comments:

Post a Comment