Mwigizaji mkongwe wa filamu nchini, Hashim Kambi ‘Mzee Kambi’ alikuwa mvumilivu na kuishi bila mwanamke kwa muda wa miaka saba mpaka alipoamua kuoa mwezi wa kumi mwaka huu.
Akipiga stori na GPL, Mzee Kambi alisema kwa muda wote huo alikuwa akishughulika zaidi na kazi kwani tayari ana watoto wakubwa na hakuona haja ya kuwa na mwanamke hadi alipoamua kumuoa mchumba wake ambaye ni raia wa Burundi aliyemtaja kwa jina moja la Hadija.
“Namshukuru Mungu kwamba amenipa mke mwema, uzuri ni kwamba hata yeye nimemkuta ana watoto aliozaa na mwanaume mwingine, tumeelewana,” alisema Mzee Kambi.
Bongo Movies
http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/mzee-kambi-nilikaa-miaka-saba-bila-mwanamke
No comments:
Post a Comment