Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama amesifia
uvaaji wa fulana wa mchezaji wa mpira wa kikapu Lebron James wakati alipokua
akifanyiwa mahojiano na gazeti la the people magazine. Rais Barack Obama
alipouliwa swali hilo nini mtizamo wake alisema nadhani ni jambo zuri kwa
mchezaji huyo na wengine waliopaza sauti zao kuwakilisha mawazo yao kwa mambo
yaliyotokea ya kuuwawa kwa Wamarekani weusi na polisi huko Ferguson jimbo la
Missouri na Brooklyn New York na baadae mahakama kuwaachia huru polisi hao
waliofanya mauaji hayo kwamba walikua wakitekeleza wajibu wao wa kazi.
I can;t Breathe ni maneno ya mwisho
aliyeongea Eric Garner kabla ya kukata roho baada ya kukabwa koo na polisi
wakati walipokua wamekwenda kumtia mbaroni.
http://lukemusicfactory.blogspot.com/
http://lukemusicfactory.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment