Arusha. Wanafunzi 344 waliomaliza darasa la saba
mwaka huu mkoani hapa wamebainika kuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.
Ofisa elimu wa mkoa, Nestory Mloka alitoa taarifa hiyo juzi katika kikao cha
elimu kilichoitishwa kwa ajili ya kuchambua matokeo ya mtihani wa darasa la saba
na kuwapangia shule wahitimu waliofaulu.
Mloka alisema kati ya walihitimu
hao ambao hawajui kusoma na kuandika, wavulana ni 163 na wasichana
181.
Alisema Wilaya ya Ngorongoro yenye wakazi wengi wafugaji wa jamii ya
Kimasai, ndiyo ina idadi kubwa ya wanafunzi hao wenye tatizo hilo wanaofikia
230.
No comments:
Post a Comment