Msanii wa filamu za Kibongo Aunty Ezekiel ‘Mama
Kijacho’.
Na Laurent Samatta/Uwazi
HUKU kukiwa na tabia kuwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wajawazito wanakuwa
na tabia za kusumbua na kubagua baadhi ya vitu, msanii wa filamu za Kibongo
Aunty Ezekiel ‘Mama Kijacho’, amesema kwa upande wake yuko vile vile na wala
hajabadilika.
Akimwaga ‘ubuyu’ na Uwazi, Aunty alisema kuwa
haoni kama amebadilika kitabia au kuwa msumbufu bali anajiona yupo kawaida
ingawa mara nyingine anakuwa anachoka sana.
“Mimba wala haijanibadili maisha kwa maana sipo
kama wanawake wengine wanavyokuwa wasumbufu, naamini kuwa nitaendelea kuwa hivi
hadi mwisho nitakapojifungua,” alisema Aunty.
No comments:
Post a Comment