Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa
pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25,
2015, alipofika kuhani kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud
aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba
wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari
yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa
ziara za kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi
Fawzia Rasheed, Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization
(Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani, leo Jumatatu 26, 2015 kuungana
na viongozi mbali mbali duniani kujadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji
chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea. PICHA NA
IKULU
No comments:
Post a Comment