Baadhi
ya waratibu mbalimbali wa Vikundi vya Benki za Kijamii VIKOBA wakimsikiliza
Meneja huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Simon Martin,alipokuwa akitoa
mafunzo juu ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti,mafunzo hayo
yalifanyika makao makuu ya vikundi hivyo vya Benki za kijamii jijini Dar es
Salaam yakiwa na lengo la kuwawezesha kujua namna ya kutumia mawasiliano katika
kuboresha shughuli zao.
Meneja
huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Simon Martin(kushoto)akimwelekeza Mratibu
wa VIKOBA International Vardiana Kamgisha jinsi ya kupata huduma rahisi za
mawasiliano kupitia simu ya kisasa aina ya smart phone wakati wa mafunzo maalumu
kwa vikundi hivyo vya Benki za Kijamii juu ya matumizi ya simu za mkononi kwa
kutumia Intaneti.Mafunzo hayo yalifanyika makao makuu ya vikundi hivyo vya Benki
ya Kijamii jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kuwawezesha kujua namna ya
kutumia mawasiliano katika kuboresha shughuli zao.
Mratibu
utekelezaji wa VICOBA Valeria Nguma(wapili toka kulia)akifafanuliwa jambo na
Meneja huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Stima Mgeni wakati wa mafunzo
maalumu kwa vikundi hivyo vya benki za kijamii juu ya matumizi ya simu za
mkononi kwa kutumia Intaneti,Mafunzo hayo yenye lengo la kuwawezesha kujua namna
ya kutumia mawasiliano katika kuboresha shughuli zao yalifanyika makao makuu ya
vikundi hivyo vya Benki za Kijamii jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment