Polisi wamuokoa chini ya ulinzi mkali, Wananchi
wamzomea, wamwita mwizi.
Mbunge wa jimbo la Segerea wilayani Ilalal,
mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Makongoro Mahanga, akiondolewa na askari polisi
kwenye ukumbi wa Anatouglou, Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo Jumatano
Januari 7, 2014, baada ya kundi la watu wenye "jazba', kutishia kumpa kichapo
kama asingeondolewa kwenye eneo hiloambalo lilitumiwa kuwaapisha wenyeviti wa
serikali za mitaa kutoka wilaya hiyo.
"Atoke, atoke, atoke" hizo ni kelele kutoka
kwa watu hawa, huku polisi wakijaribu kuwatuliza
Dkt. Mahanga, akiwa anatoka kwenye ukumbi huo
huku polisi wakiwa "hawachezi mbali"
Vurugu katika zoezi la kuapisha wenyeviti
wateule wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji zimepamba moto, ambazo
zimesababisha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, kujikuta
akizomewa na wananchi na kusababisha zoezi hilo katika baadhi ya mitaa na
vitongoji katika maeneo mbalimbali nchini kukwama.
Dk. Mahanga, ambaye pia ni Mbunge wa Segerea (CCM) alikumbwa na masaibu hayo wakati wa hafla ya kuapisha wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa katika Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na hivyo, kulazimika kuondolewa katika ukumbi wa Halmshauri ya Manispaa ya Ilala wa Anartoglou chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Kabla ya kukumbwa na mkasa huo, Dk. Mahanga alifika katika ukumbi huo ili kushuhudia kuapishwa kwa viongozi wa serikali za mitaa wanaotoka katika jimbo lake.
Katika eneo hilo, kulikuwako na mchanganyiko wa watu, wakiwamo wapambe waliokuwa wakishuhudia zoezi hilo.



No comments:
Post a Comment