Staa wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amefungukia msimamo wake juu ya mwandani wake
wa zamani, Wema Sepetu ‘Madam’ kwa kusema kuwa kamwe hawezi kumrudia
tena.
Licha ya Diamond
kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya vipindi, kuna wakati waliwahi
kumwagana kisha kurudiana na hakuna aliyewahi kutoa tamko zito lakini safari hii
Diamond amesema ndiyo basi tena!
Kwa mujibu wa chanzo
makini cha gazeti la Risasi kilicho karibu na staa huyo, mara kwa mara Diamond
amekuwa akijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake na kusisitiza kwamba pamoja na
kuwa maisha ya sasa huendeshwa kwa msingi wa fedha lakini hata kama ‘atafulia’
kiasi gani, ni bora afe maskini kuliko kurudiana na Wema.

No comments:
Post a Comment