JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu:
255-22-2114615,
211906-12
Nukushi: 255-22-2116600 |
|
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX
9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
WATANZANIA
WALIOKUWA AFRIKA KUSINI WAMEREJEA NYUMBANI
Kundi la
Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 26 Aprili,
2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza
kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.
Watanzania hao
walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini
Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao
lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Wakati huo huo,
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania
wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg.
Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa
hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.
MWISHO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa,
25 Aprili 2015
No comments:
Post a Comment