Dar,
Mikoani. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwamo vyuoni,
ofisi za umma na kwenye migahawa mikubwa baada ya kuwapo kwa hofu ya shambulizi
la kigaidi katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.
Hofu
hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Chuo Kikuu cha Garissa, cha nchini Kenya
kushambuliwa na kusababisha vifo vya wanafunzi 148.
Baada
ya shambulizi hilo, kumekuwa na ujumbe mfupi wa simu unaoendelea kusambazwa
ukionya kuwapo kwa shambulizi katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment