Wandugu TYK: UJUMBE KUTOKA KWA MWENYEKITI MARTIN ASSIS

Kwa niaba ya familia ya Baba Clemence Masumbuko Martin Mushi wanapenda kuwajulisha ya kwamba kijana wao mpendwa Maximilian Clemence Mushi anataraji kukamilisha sakramenti ya ndoa takatifu ambapo kwa mapenzi ya Mungu ndoa hiyo inataraji kufungwa siku ya Jumamosi tarehe 04-07-2015 katika Parokia ya Bikira Maria - Mbezi, D'salaam.

Kuelekea kilele cha ufanikishaji wa siku hiyo, familia ya Baba Clemence inakuomba kuudhuria kikao cha kwanza cha maandalizi ya kufanikisha tukio hili muhimu kitachofanyika siku ya Jumamosi tarehe 18-04-2015 saa 11:00 jioni.

Jina ukumbi na ramani ya kufika hapo Ndg yetu Mwl Odilia "Oddy" atawasilisha punde.

Tafadhali unaombwa ukipata ujumbe huu mjulishe na mwenzako.

TYK

Sent from my BlackBerry 10 smartphone.

No comments:

Post a Comment