Polisi nchini Italia
wanasema kuwa wamewakamata watu 18 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Islamic State
kutoka nchini Afghanistan na Pakistan katika oparesheni kubwa ya kupambana na
ugaidi.
Wanasema kuwa wawili kati
ya washukiwa hao wanaaminiwa kuwa walinzi wa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda
Osama Bin Laden na wengine wanashukiwa kuhusika kwenye mashambulizi nchini
Pakistan likiwemo shambulizi lililotokea kwenye soko la
Peshawar.
Oparesheni hiyo ilikuwa
imeendeshwa kwenye kisiwa cha Italia cha Sardina .
Polisi walisema kuwa kundi
linalofanyiwa uchunguzi lilikuwa limewapangia wanachama wake kuingia nchini
Italia wakiwa na vyeti vya kufanya kazi au kama watafuta hifadhi.
No comments:
Post a Comment