Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu ya kwenye daladala.


1.Yatima hadeki

2.Utamu wa chips mimba

3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni

4. Usiyempenda kaja

5. Kobe hapimwi joto

6. Acha kazi uone kazi kupata kazi

7. Ukichezea koki utalowa

8. Heshima pesa kipara kovu tu!

9. Mtumbwi hauna saitmira.

9. Silaha pesa bastola mzigo

10. Hata uoge mjini huendi

11. Chezea mshahara usichezee kazi.

12. Ukiona manyoya ujue keshaliwa

13. Ikisimama Panda

14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe

15. Njia ya chooni haioti nyasi

16. Likizo ya maskini ugonjwa

17. When i grow up i want to be a scania

18. Hata bibi alikuwa binti

19. Kisigino hakikai mbele

20. Kama mapenzi pesa kaolewe na benki

21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi

22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee

23. Paka haishi kwa msela

24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa

25. NIPO NIPO KWANZA

26. Mchana nzi ucku mbu

27. Usimshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake

28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako

29. Supermarket hawauzi mkaa

30. We nisubiri mi nakungoja.

31. Zetu dagaa kuku tamaa

32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki

No comments:

Post a Comment