
Mwanzoni
mwa mwaka huu (2015) mrembo na muigizaji wa filamu, Elizabeth “Lulu” Michael
aliwa-surprise watu wengi pale alipomzawadia mama yake nyumba aliyojenga Kimara,
jijini Dar es- Salaam.
Lulu
alimpa zawadi hiyo mama yake kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa January,
2015.
Je Lulu
aliwezaje kufanya mambo makubwa kama hayo katika umri mdogo na kwa kipato cha
kuigiza peke yake? Hayo ni maswali ambayo wengi walijiuliza, kiasi cha kuwafanya
wengine waamini kuwa labda amehongwa.
Lulu
amesema kuwa nyumba hiyo alianza kuijenga kidogo kidogo miaka minne iliyopita
kwa kile alichokuwa anakipata kupitia kazi yake ya uigizaji, lakini watu wengi
hawakufahamu mpaka siku alipoitoa kama zawadi kwa mama yake.
“Kiukweli
ile nyumba nimeanza kujenga nikiwa bado mdogo sana, ni nyumba ya chini ya
kawaida lakini nilikuwa najenga kidogo kidogo, kwamba leo nikipata laki nampa
mama leo kaongezee hiki…kwahiyo ni kwasababu mtu hajui atashangaa Lulu kapata
wapi hela za vuuup, lakini ni kitu ambacho kimeenda kidogo kidogo imechukua hata
miaka minne..kwahiyo mtu atashtuka kwasababu ameiskia leo sasa ndo hivyo mtu
ataanza kusema kahongwa hajui background.” alisema Lulu kupitia The Sporah Show.
No comments:
Post a Comment