Kila First Lady wa Marekani huwa anachukua jukumu fulani ambalo sio la kiserikali sana pindi mumewe anapokuwa madarakani. Kwa Michelle Obama, masuala ya afya hususani kwa vijana na watoto bila shaka ndicho kitu ambacho amedhamiria kukisimamia zaidi.
Hivi sasa anayo kampeni ambayo imepewa hashtag ya #GimmeFive ambayo imelenga kusherekea miaka 5 tangu alipoanzisha kampeni ya Let’s Move. Anataka kila mtu aliyepo kwenye mitandao ya kijamii kusema au kuwashirikisha wengine katika mambo 5 anayoyafanya ili kuwa na afya njema.
Tizama video ambayo ameiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram. Mwanamama yupo fit hatari. Tayari mumewe,Barack Obama na mastaa wengine kama Beyonce, Nick Cannon na Hugh Jackman wameshamuunga mkono.

No comments:
Post a Comment