Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono mamia ya wana CCM na wananchi wa Manispaa ya Lindi, waliojitokeza kwenye ofisi za chama mkoani humo Juni 17, 2015. . Mheshimiwa Lowassa ambaye amechukua fomu kuomba chama kimteue kuwani urais wa Tanzania Oktoba 25, 2015, alijizolea wana CCM 3,279.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa, akisalimiana Mwana CCM huyu aliyejitokeza kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Mtwara mjini, Juni 17, 2015. . Mheshimiwa Lowassa ambaye amechukua fomu kuomba chama kimteue kuwani urais wa Tanzania Oktoba 25, 2015, alijizolea wana CCM 3,500.
Mwana CCM huyu wa mkoani Mtwara ambaye alikuwa miongoni mwa waliojitokeza kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiomba dua iliyokuwa ikiongozwa na kaimu kadhi wa mkoa huo, Sheikh, Kassim Kuneng’eneka, kumuombea Mh. Lowassa, baada ya kupata wadhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Mtwara Juni 17, 2015. Mheshimiwa Lowassa alipata jumla ya wadhamini 3,500.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akipaya mapokezi ya WanaCCM Tanga.
Wazee wa Tanga wakimpigia Dua Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akikumbatiana na Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa mkoa wa Tanga Juni 17, 2015, kutafuta wadhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba CCM imteue kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa ,kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ambaye awali alikuwa akitokea mikoa ya Mtwara na Lindi, alikozoa jumla ya wana CCM waliomdhamini 6,779, pale Tanga alivunja rekodi ya wadhamini baada ya kuwapata zaidi ya 24, 000. 9Picha zote na K-VIS MEDIA)
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Mzee Harith Bakari Mwapachu, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa mkoa wa Tanga Juni 17, 2015, kutafuta wadhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba CCM imteue kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa ,kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ambaye awali alikuwa akitokea mikoa ya Mtwara na Lindi, alikozoa jumla ya wana CCM waliomdhamini 6,779, pale Tanga alivunja rekodi ya wadhamini baada ya kuwapata zaidi ya 24, 000. (Picha zote na K-VIS MEDIA).