Ndugu
Marafiki,
Baadhi yenu mnafahamu kwamba ndugu na
rafiki yetu, Adolf Simon Kivamwo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI Tanzania (AJAAT), ni mgonjwa na anasumbuliwa saratani ya utumbo mpana toka mwaka 2012. Tangu wakati huo, amekuwa akitibiwa na kuhudhuria matibabu na kliniki katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (OCRI). Wataalamu wa tiba ya saratani
wanamti
-
bia
kwa dawa mchanganyiko dawa tofauti kwa
mtindo wa chemotherapy. Tiba hizo
zinalenga kudhibiti kasi ya kuenea kwa ugonjwa kwa kushauriana na mgonjwa. OCRI ni taasisi inayoendeshwa na
serikali inatoa tiba ya saratani bila malipo kwa
wagonjwa. Hata hivyo, kutokana na uhaba wa rasilimali, taasisi hiyo inapokea kiasi kidogo au kutopokea dawa muhimu kutoka Bohari ya Dawa ya Serikali (Medical Stores Department - MSD). Hali hiyo
ni jambo la kawaida kwenye hospitali za
serikali. Kutokana na hali hiyo, wagonjwa wanalazimika kununua dawa kwenye maduka binafsi na kuzipeleka OCRI
kwa ajili ya tiba. Hiyo ndiyo sababu Simon amekuwa akitumia wastani wa Tshs 500,000/ - (laki tano) kwa wiki kwa ajili ya kununua dawa za tiba za chemotherapy. Amefanya hivyo kwa kuuza mali zake na kutokana na
michango ya marafiki kwani hana bima ya
afya kugharamia matibabu yake. Ni miaka mitatu sasa hali yake ya afya si ya
kuridhisha. Afya yake imezidi kudhoofu siku baada ya siku. Na sasa hawezi kufanya shughuli zake mwenyewe kwani muda mwingi hulala nyumbani kwake Mbezi na kuhudhuria matibabu Ocean Road kila baada ya wiki mbili. Kwa bahati mbaya, Simon amekuwa akikatisha dozi za tiba kwa kukosa fedha! Ugonjwa huo umekuwa ukimshambulia kwa kumsababishia maumivu makali, hali inayomfanya kulazwa hospitali mara
kwa mara kutokana na maumivu makali ya tumbo! Baada ya kugundua mwenzetu Simon anateseka akiugulia kitandani, sisi marafiki zake wengi ambao ni wana habari kupitia mtandao wa Facebook tumekuwa tukipeana taarifa za maende
-
leo ya afya yake na kuendesha mchango wa
kumsaidia. Michango hiyo ndiyo ilimwezesha kurejea kwenye matibabu Ocean Road, ambapo madaktari walim
-
taka pia afanye vipimo vya CT-Scan katika hospitali binafsi ili kuangalia ukubwa wa tatizo lilivyo. Michango hiyo iligharamia CT-Scan. Sambamba na michango, pia tulianza jitihada za
kuwasiliana na viongozi serikalini ili kutafuta uwezekano wa kumpeleka nchini India kwa ajili ya matibabu. Wizara ya afya iliahidi kutoa ushirikiano endapo maoni na ushauri wa wataalamu wa OCRI ungeridhia hilo. Sasa majibu ya vipimo vya CT Scan yamepatikana na imeshauriwa kwamba kwa sasa si busara kumpeleka India, kwani anapaswa kuendelea kwanza na dozi ya chemotherapy ambayo aliikatiza. Na
hivyo atalazimika kupata dozi 10 za Chemotherapy, kuanza tarehe 20, ambapo atakuwa akipata dawa hizo kila baada ya wiki mbili. Mpaka kumalizika kwa
mzunguko tutahitaji jumla ya shilingi shilingi milioni 5. Hii ndiyo sababu tunaandika kwenu wadau na marafiki kuomba msaada wa fedha. Huu ni msaada mkubwa kwa Simon Kivamwo aliyewahi kufanya kazi akiwa mwandishi wa habari katika Kam
-
puni ya The Guardian Limited kabla ya kuanzisha AJAAT. Na kama inavyojulikana, AJAAT
ni moja ya mdau muhimu katika
mwitikio wa UKIMWI kupitia kwa mafunzo
kwa waandishi kuhusu uandishi sahihi wa habari na makala za UKIMWI. Kivamwo amejitolea kwenye hili maisha yake yote, japo yeye mwenyewe haishi na virusi vya
UKIMWI. Tunaomba mchango wako ndugu na rafiki yetu. Tuma mchango kwa namba hii:Simon Kivamwo 0767300219 . Kwa Mawasiliano zaidi kuhusu mgonjwa karibu:Benjamin ThompsonEmail: benjathom@gmail.comSimu,Whatsapp, sms au piga simu:
0787303067/0767383067
Ungana na Simon Kivamwo kupambana na Kansa ya Utumbo
No comments:
Post a Comment