
Matapeli waliotambulika kwa majina ya Innocent Joseph na Kakamba, Iden na Wenzao wawili, wanaotokea Kampuni ya Utafiti ya Research Solution Africa, wamekuwa wakifanya kazi ya kupokea Tenda za Research na watu wamekuwa wakilipwa kwa siku, usiku na mchana ikitegemea na mteja anayefadhili zoezi hilo la utafii.
Mfano miongon mwa benki zinazodhamini ni World Bank ambapo huwa wanawalipa watu kiasi cha Sh. 25,000/= kwa Mkoa wa Dar es Salaam, na iwapo watasafiri mikoani vijini watalipwa kiasi cha Sh. 65,000/=.
Watajwa, hapo juu hivi sasa wanatafutwa kutoka na matukio kadhaa ya kitapeli waliokwisha yafanya siku za hivi karibuni ambapo mwezi uliopita walitangaza tenda ya 'Research Vacancy' na kukusanya wanafunzi wengi tu na wafanyakazi kadhaa waliofika kujiandikisha ili kushiriki mafunzo hayo kwa ajili ya kupewa safari hizo za kwenda kufanya utafiti mikoani.
No comments:
Post a Comment