WATU wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakituhumiwa kughushi, kutengeneza tovuti bandia na mifumo ya mtandao kwa kutumia majina ya baadhi ya viongozi wa Serikali, likiwemo la Rais Jakaya Kikwete na taasisi kubwa hapa nchini.
Washitakiwa hao ni Patrick Natala na Maxmillian Msacky waliofikishwa mahakamani hapo jana ambapo Mawakili wa Serikali, Theophil Mutakyawa akisaidiwa na Wakili Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Johannes Kalungura, waliwasomea washitakiwa hao mashitaka 10.
Washitakiwa hao wanadaiwa kati ya Januari na Aprili, 2014, walitengeneza tovuti bandia…
No comments:
Post a Comment