KWA STAILI HII KIPINDUPINDU HAKITATUACHA

 Maji ya shida, umeme kwa mgao, internet kwa vifurushi, daresalama mambo yake si salama, haya ndio yanayowakuta wakaazi wa daresalama. shida inapotokea wengine wananufaika, wengine wanahasirika, waburuta vitoroli kwao inakuwa neema, tenda za kuchota maji zinawaongezea kipato, lakini usalama wa maji hayo hauna uhakika wapi wameyapata, ugumu wa jibu  wasuali hilo, inawafanya wengine wakaze buti wakayatafute maji popote yalipo kwa gharama yoyote. PICHA NA VIJIMAMBO/KWANZA PRODUCTION
Pamoja na taghadhari ya tishio la gonjwa hatari kipindupindu, kamera yetu ya vijimambo katika mitaa ya Likoma na Kongo iliweza kunasa maandalizi ya chakula pembeni mwa barabara ambayo iko busy na kwa watu na magari vumbi likiruka, bila ya kuwa nakinga yoyote ya vumbi hilo lisiingie katika chakula hicho

No comments:

Post a Comment