HII kali! Mtumishi mmoja anayetumikia nafasi ya ulinzi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro (St. Peter) lililopo Oysterbay jijini Dar (jina halikufahamika), amenaswa katika chumba cha kuhifadhia chakula kinachoitwa Mwili wa Kristo (ekaristi) ndani ya kanisa hilo.
Kwa mujibu wa mtawa (sista) mmoja wa kanisa hilo aliyeomba hifadhi ya jina, awali tabia ya wizi wa chakula hicho ambacho ni mkate (ekaristi), divai (mvinyo) na vifaa vingine, mali ya kanisa ilikithiri kanisani hapo mpaka kufikia hatua ya baba paroko kuamuru kufungwa kwa kamera ya Closed-Circuit Television (CCTV) ili kuweza kumnasa mwizi huyo.
KUNA WALIOKATWA MISHAHARA
Sista huyo aliendelea kuanika kuwa, kutokana na kuibwa kwa vitu hivyo mara kwa mara, tena vikiwemo na vifaa vya muziki na vitu vingine vya thamani, baadhi ya wafanyakazi walikatwa mishahara yao ili kuwaonesha kuwa, uongozi haukubaliani na wizi huo wa mara kwa mara ambao uliashiria dalili ya uzembe.
No comments:
Post a Comment