Ashura Ramadhani anayedaiwa kucharangwa mapanga na mumewe.
Na Haruni Sanchawa
WIVU! Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Abdallah, mkazi wa Gongo la Mboto, Ilala jijini Dar es Salaam, anadaiwa kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili mkewe Ashura Ramadhani kwa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili juzi kuwa Abdallah baada ya kufanya unyama huo, alikimbilia kusikojulikana na jeshi la polisi linamtafuta ili akabiliane na sheria.
Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto imethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo afisa mmoja alisema wawili hao walipeleka shauri lao hapo ambapo baada ya kusikilizwa, walikubaliana kila mmoja aishi kwenye chumba chake, uamuzi ambao hata hivyo, mwanamke aliupinga vikali.
No comments:
Post a Comment