Baby Madaha aanguka chooni, avunjika mguu

IMG_8153Msanii wa filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha akiwa na  P.O.P mguuni.
Musa mateja
MSANII wa filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha hivi karibuni alipata majanga baada ya kuanguka chooni na kuvunjika mguu wa kulia, Amani lina taarifa zote.
Tukio hilo lilitokea nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar ambapo staa huyo alitoka kwenye matembezi yake usiku wa manane akiwa amepiga ‘mtungi’ wa kutosha.
Inadaiwa kuwa, alipofika kwake alihitaji kwenda bafuni kuoga. Hata hivyo, alianzia chooni kwanza na kutokana na miguu kukosa stamina kwa ‘ulabu’, alijikuta akiteleza na kudondoka chini kisha kuvunjika mguu huo.
IMG_8152
Muonekano wa mguu huo uliovunjika.
Amani lilimsaka msnaii huyo ili kuzungumza naye kuhusu madai hayo ambapo alikiri kupata majanga.Baby Madaha alisema msala huo ulimfika majira ya saa 10 alfajiri (siku hakumbuki) akitoka kwenye kujirusha ambapo siku hiyo pombe zilimkoma kwa kufakamia kila aina.
“Naamini kufakamia kwangu pombe nyingi ndiyo kuliniponza. Sijawahi kupata maumivu makali kama haya maana baada ya kudondoka chini nilijisikia sina nguvu wala sikuweza kusimama, nikalazimika kuukanyagia mguu wangu.
“Ilipofika asubuhi nilijikaza kwenda Hospitali ya AAR iliyopo Kijitonyama (Dar) ambapo walinipiga X-Ray na kungundulika kuwa, mguu wa kulia ulivunjika, hivyo nikafungwa mhogo (P.O.P),” alisema Madaha.
IMG_8144Alisema kwa sasa (Jumanne iliyopita), anaendelea vizuri sana na anawashukuru madaktari wa AAR kwani awali yeye alijua mguu huo aliteguka tu na ungetengemaa muda wowote.
“Da! Lakini yote maisha, leo tambarare, kesho mlima. Binadamu huwezi kuishi katika tambarare siku zote wala mlima siku zote. Najua hili hogo litatoka, nitadunda kama kawa,” alisema mrembo huyo.

No comments:

Post a Comment