Polisi ‘yawatumbua majipu’ trafiki, yabadili mfumo

By Waandishi Wetu, Mwananchi

Dar/Mikoani. Jeshi la Polisi limefanya mabadiliko kadhaa katika Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kuwahamisha baadhi ya askari wake huku wengine wakishushwa vyeo au kuachishwa kazi kutokana na makosa mbalimbali makubwa yakiwa malalamiko ya kuwaonea wananchi, rushwa na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara.

Kamanda wa kikosi hicho, Mohamed Mpinga akizungumza wiki iliyopita alisema ili kupunguza rushwa na kuingiza mapato, kikosi hicho kimeanzisha mfumo mpya wa kulipa faini wa kutumia mashine za EFD, ambao awali, ulifanywa kwa majaribio na kuonyesha mafanikio licha ya kasoro kadhaa zilizojitokeza.

Dar es Salaam

Wakati hatua hizo zikichukuliwa, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imeshawabadilisha kazi wakaguzi saba na askari wa vyeo mbalimbali 157 wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambao utendaji kazi wao umeonekana kukosa tija.

No comments:

Post a Comment