Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo ametimiza mwezi mmoja tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo huku akiweka rekodi ya kuokoa kiasi cha Sh997.4 bilioni (karibu Sh 1trilioni) ambazo zilikuwa zitumike kwa matumuzi yasiyo ya lazima, na ukwepaji kodi.
Sh997.4 bilioni zilizookolewa zitaweza kutumika kununua magari ya wagonjwa, kujenga zahanati, kujenga barabara za lami, kununua madawati, kujenga vyumba vya madarasa, kuchimba visima, kununua mashine za uchunguzi wa magonjwa, magari ya wanafunzi, pikipiki kwa maofisa kilimo, mikopo ya elimu ya juu au kujenga viwanja vya michezo kadri Serikali itakavyoelekeza.
Dk Magufuli aliapishwa Novemba 5 katika hafla iliyofana na alianza kazi ya kutafuta na kuziba mianya ya upotevu wa fedha Novemba 6 alipotembelea Hazina. Katika mazungumzo ya watendaji wa wizara hiyo Rais Magufuli alipiga marufuku safari zote za nje na kwamba zitakuwa zinaruhusiwa kwa kibali maalumu.
No comments:
Post a Comment