Wafanyabiashara mbalimbali wamedai kwamba sikukuu ya Christmas ambayo husherekewa kila mwaka ifikapo Desemba 25 kwa mwaka huu imedorola huku shamra shamra zilizokuwepo miaka mingine zikiwa zimepungua kwa kiasi kikubwa.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya wafanya biashara katika soko la Kariakoo, Buguruni pamoja na Ilala wote kwa pamoja wamesema kuwa Christmasi ya mwaka huu mauzo yako chini ukilinganisha na misimu mingine ya sikukuu hiyo kubwa Duniani.
Jakson Haule mfanyabiashara wa Nguo Kariakoo jijini Dar es salaam amesema sikukuu ya Christmasi ya mwaka huu haina mvuto kwa kuwa wateja sio wengi kama ilivyokuwa katika miaka mingine ambapo muda huu kulikuwa na shamra shamra na hamasa kubwa ya wananchi kujiandaa kwa kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Mwajuma Hamisi mfanyabiashara wa vyakula amesema kwamba wafanyabiashara wamepata mshangao mkubwa mwaka huu kwa kuwa mauzo yamekuwa kawaida sana utadhani hakuna sikukuu kubwa kama hiyo itakayokuwa siku ya Ijumaa desemba 25.
Peter Jumanne mfanyabiashara wa soko la Buguruni amesema kwamba miaka ya nyuma kulikuwa na kundi kubwa la wananchi kutoka maeno mbalimbali walikuwa wakimiminika kununua bidhaa soko la Buguruni kwa kuwa soko hilo ni nafuu sana lakini kwa mwaka huu imekuwa kawaida sana.
“Wafanyabiashara tunashangaa kama huu ni msimu wa christamas au hakuna Christmas, kwa kuwa imepooza sana hakuna mishe mishe tulizo zoea” Alisema Bw.Peter.
Mfanyabiashara mwingine ni Rajab kutoka soko la Ilala ambaye amesema wafanyabiashara wanahisi kushuka kwa mauzo kume endana na kasi ya Rais John Magufuli kufuta baadhi ya mambo serikalini yaliyopelekea wafanyakazi kujipatia fedha ya ziada hivyo sasa wameamua kubana matumizi ili fedha hiyo itumike katika mambo msingi pekee.
Kila mwaka ifikapo tarehe 25 desemba wakristo Duniani kote huungana kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana yesu kristo.
No comments:
Post a Comment