Waziri akuta ‘ofisi nzima’ wako likizo

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
By Raymond Kaminyoge, Mwananchi

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amefanya ziara ya kushtukiza Ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba za Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukuta zaidi ya nusu ya watendaji wake wako likizo.

Naibu Waziri huyo aliwasili ofisini hapo jana saa 8.30 mchana na kupokewa na mtunza kumbukumbu, Bahati Kassim ambaye ni mtumishi pekee aliyekuwapo ofisini.

Baada ya kusaini kitabu cha wageni, naibu waziri aliuliza waliko watumishi wengine.

Naibu Waziri: Watumishi wengine wako wapi?

Bahati: Wako likizo na mmoja ametoka kikazi.

No comments:

Post a Comment