Baadhi ya wakazi wanaoishi mabondeni wakiwa mahakamani hapo.Wakazi wa maeneo ya mabondeni wakiwa tayari kusikiliza shauri la zuio lao la kusitisha bomoabomoa mahakamani hapo.Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia (katikati) akiwa na wakili wake kabla kesi kusikilizwa.
KESI ya kupinga bomoabomoa iliyofunguliwa na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF) katika Mahakam Kuu kitengo cha Ardhi jijini Dar es Salaam imesikilizwa leo na kuahirishwa hadi kesho.
Mtulia (kushoto) akijaribu kuzungumza na wananchi waliofika mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilipewa Na. 822 ya mwaka 2015 na kupangiwa jaji wa kuisikiliza, Penterine Kente, huku upande wa walalamikaji ukisimamiwa na wakili Abubakar Salim.
Hali ilivyokuwa nje ya mahakama hiyo.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuahirishwa kesi hiyo, Mtulia akiwa na wakili wake, Abubakar Salim, amesema kuwa jumla ya watu nane wamewawakilisha wakazi wa maeneo tofauti ya mabondeni, huku akisema kuwa lengo si kufungua kesi kupinga ubomoaji wa wakazi wa mabondeni bali wananchi hao watendewe haki ikiwa ni pamoja na kupewa viwanja walivyoahidiwa.
Hali halisi ilivyokuwa.
Naye Kente mara baada ya kusikiliza pande zote mbili ameahirisha kesi hiyo hadi kesho kufuatia upande wa mawakili wa serikali kudai kuwa serikali ilishatoa maamuzi ya wakazi wa mabondeni kuhama maeneo hayo na akadai maamuzi ya shauri la zuio la kubomoa nyumba zilizojengwa bondeni yatatolewa kesho saa tano baada ya madai ya wakili wa serikali kudai zuio lao limecheleweshwa.
NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment