Saluni za ngono, kimenuka Dar

MHUDUMUMuhudumu wa mija ya saruni akijificha kuikimbia kamera.

Issa Mnally na Chande Abdallah, IJUMAA
DAR ES SALAAM: Kweupee! Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers, wiki hii ilizama mitaani kufanya uchunguzi kufuatia madai kuwa, licha ya oparesheni zinazofanywa na OFM kuhusu saluni za huduma ya masaji kutumika kufanyia ngono, bado wahusika hawataki kuachana na tabia hiyo, twende na Ijumaa.
MAENEO YALIYOIBUKIWA
OFM ilizama baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar, hususan Sinza, Kinondoni, Mikocheni na Makumbusho ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kwamba, yameota kutu kwa tabia hiyo.
KILICHOBAINIKA
OFM ilibaini kuwa, sehemu hizo zinatoa huduma ya masaji lakini baadhi ya wahudumu ambao ni wanawake wanakiuka kwa kutoa huduma ya ngono kwa wateja wanaume.
Paparazi wetu mmoja alizama ndani ya saluni iliyopo Sinza Palestina, Dar na kuulizia kama anaweza kupata huduma ya kuchuliwa ‘masaji’ na ya ngono:
“Unaweza anko. Hapa huduma zote zipo. Ni wewe tu! Lakini huduma ya masaji, unalipia elfu sitini (60,000) mapokezi, huduma ya ngono unanilipa mimi chumbani. Kazi kwako anko,” alisema mhudumu aliyekutwa
2WANAFANANA
Majibu ya mhudumu huyo hayakutofautiana na ya masaji nyingine zilizopo Mlimani City, Mikocheni na Makumbusho ambao walisema malipo ya huduma ya ngono yanafanywa chumbani kabla ya makasheshe.
MAZINGIRA YAKE
Katika masaji zote hizo, eneo la mapokezi kuna baa ndogo zilizosheheni pombe kali na vinywaji laini kwa ajili ya wateja wanaosubiri huduma au walio vyumbani wakihudumiwa.
OFM LATINGA SERIKALINI
Baada ya kushuhudia hayo, OFM ilifika kwa Afisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Zahoro Rashid na kutaka kujua sheria zinasemaje kuhusu usajili wa saluni hizo.
SALUNI-3-001
Mteja aliyenaswa kwenye moja ya saruni.
TAMKO LA SERIKALI
Akizungumza na OFM, afisa huyo, kwanza alikiri kusikia fununu kuwa, baadhi ya saluni, Dar zimekuwa madanguro.
Zahoro akaweka wazi sheria ya usajili wa saluni hizo kuwa ni marufuku kuuza pombe ndani kwani leseni zao haziruhusu kileo chochote. Akaiomba OFM kuwafichua wenye saluni ambao wanavunja maagizo hayo.
“Tunawaomba sana nyinyi waandishi mtusaidie kuzifichua hizo saluni ili tuzichukulie hatua husika ikiwemo kuzifutia leseni za biashara na kuwapeleka mahakamani,” alisema afisa huyo.
SALUNI-5-001
Vitendea kazi vikiwa kwenye kabati.
HUDUMA YA NGONO
Baada ya hapo, OFM ilimwambia afisa huyo kuwa, kuna picha zilipigwa mwishoni mwa mwaka jana (angalia Uk. 24) baada ya kumnasa mhudumu na mteja wakiivunja amri ya sita ya Mungu ndani ya saluni moja iliyopo Mlimani City. Sikia tamko la afisa huyo.
“Loo! Hilo ndiyo baya zaidi kuliko yote. Tena nawashukuru sana jamani. Ni kinyume cha sheria za usajili wa saluni za masaji kwa wahudumu kugeuza eneo hilo kuwa la kufanyia ngono.
Tukiwakamata ni mahakamani tu.
“Serikali ya sasa ipo sambamba nao, wajue kwamba, kama walizoea tabia hiyo, sasa kimenuka!

No comments:

Post a Comment