BASI LA SIMBA MTOTO LAGONGANA NA LORI WILAYANI KOROGWE MKOANI TANGA LEO ASUBUHI

Ajali imetokea mkoani Tanga asubuhi hii wakati Basi la Kampuni ya Simba Mtoto ya Tanga lilipogongana na Lori uso kwa uso katika eneo la Pangamlima Wilayani Korogwe mkoani humo, taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu 10 wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya atika ajali hiyo.

Mtandao huu bado unaendelea kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu ili kupata idadi kamili ya waliopoteza maisha.Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi-AMIN

No comments:

Post a Comment