Flora Mvungi: Sitaacha Muziki

FloraMvungi2
Flora Mvungi ‘H Mama’
Na Chande Abdallah
Msanii wa kike anayekipiga Bongo Muvi na Bongo Fleva, Flora Mvungi ‘H Mama’ amefungukia madongo anayopigwa na wasanii wenzake kuwa ameingia kwenye muziki kwa kubipu na kudai kuwa bado yupo kwenye fani hiyo.
Akipiga mbili tatu na paparazi wetu, H Mama alisema kuwa anajiandaa kuachia hewani ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mama Alisema ambayo ina mahadhi ya mduara ili kuendeleza makali yake kwenye fani yake ya muziki.
“Nani? Mimi siwezi kuacha muziki hao wanachekesha tu, hapa nilipo naandaa ngoma yangu mpya nimeifanya kwenye Studio za Mo Fire,” alisema Flora.

No comments:

Post a Comment