Jengo Ghorofa 16 Laanza Kuvunjwa Indra Gandhi, Dar

uploadfromtaptalk1454391415448IMG_0511Jengo la Ghorofa 16 linaloandaliwa kwaajili ya kubomoa.IMG_0485Alama zinazotoa tahadhali kwa watumiaji wa barabara hii wakiwa wakiwa wamewekewa tahadhali kwaajili ya kuvunjwa kwa gharofa la Ghorofa 16 lililopo mtaa wa Indra Ghandi jijini Dar es Salaam.
IMG_0497Mafundi wakiwatoa vyuma kupisha ubomoaji wa jengo la ghorofa 16 lililopo katika mtaa wa Indra Ghandi jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 lililopo katika Mtaa wa Indra Gandhi kabla halijaleta maafa, kazi ambayo imeanza leo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Patty Interplan iliyopewa kazi hiyo kwa gharama ya Sh1 bilioni, Waameanza utaratibu wa kubomoa. Mngulumi alisema gharama za ubomoaji zitalipwa na mmiliki wa jengo hilo ambaye ni Ali Raza Investment.
“Mtaa wa Indira Gandhi na Morogoro una watu wengi hivyo ghorofa likiwa limejengwa chini ya kiwango linaleta wasiwasi kwa wapitanjia,” alisema Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omar Kumbilamoto .
“Unajua wakati wa kubomoa hatari yoyote inaweza kutokea hivyo familia nyingi zimehama kwa ajili kujiepusha na maafa ambayo yanaweza kutokea,” alisema mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment