Kisa utajiri wenye maswali, Zari atajwa freemason

ZARI47817
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’
Stori: Musa mateja, Wikienda
Dar es Salaam: Mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameorodheshwa kwenye listi ya watu maarufu nchini Uganda ambao ni wanachama wa jamii ya siri ya Freemason kisa kikielezwa kuwa ni utajiri alionao wenye maswali mengi.
Habari kutoka Kampala, Uganda zilizoripotiwa hivi karibuni zilieleza kwamba, mwanamama huyo ana ukaribu mkubwa na matajiri wa Nigeria ambao wanaaminika kuwa utajiri wao ulitokana na kuwa ‘memba’ wa mtandao huo mkubwa duniani.
zari_3Gari la Zari.
Ilidaiwa kwamba, Zari amekuwa akifanya kufuru ya fedha zinazowashangaza wengi, kuwa kwa muziki au biashara gani anazofanya zinazomuingizia mkwanja mrefu kiasi cha kumiliki magari ya kifahari kama Lamborghini na Hummer ambayo yote ameyaandika majina yake badala ya namba za usajili.
Katika habari hiyo, wengine waliotajwa ni pamoja na aliyekuwa mumewe aliyezaa naye watoto watatu, Ivan Semwanga, wachungaji maarufu nchini humo na wanamuziki kama Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’ na Bebe Cool.
Zari anayemiliki hoteli ya kifahari iliyopo kwenye Mtaa wa Kagwa, Kampala nchini Uganda, anasemekana kumiliki vyuo vya urembo na maduka ya vipodozi nchini Afrika Kusini huku akijiingizia mkwanja kupitia shoo zake za Zari All White Party anazozifanya kwenye nchi za Afrika Mashariki za Uganda, Tanzania na Kenya.
Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Zari hakupatikana badala yake aliyezungumzia ishu hiyo ni mpenzi wake, Diamond ambaye alisema kuwa mama mtoto wake ana miradi mingi na siyo kama wanawake wa mjini ambao wanabweteka badala ya kutafuta mkwanja.

No comments:

Post a Comment