Jeshi la Polisi kitengo cha majini limekamata tani zipatazo 20 za mafuta ya dizeli yaliyokuwa katika Jahazi lililokuwa kando ya bandari ya Dar es Salaam likijiandaa kwa safari ya kwenda Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo hicho cha Polisi cha Wanamaji, Bw. Mboje John Kanga amesema watu watano wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi zaidi unaendelea.
No comments:
Post a Comment