Milionea Mtoto Akamatwa Dar

tikoLwitiko Adamson Mwakasala ‘Tiko’
Stori: Makongoro Oging’  na Issa Mnally, UWAZI
DAR ES SALAAM: Tumbuatumbua majipu ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ inazidi kushika kasi nchini ambapo si serikalini tu, hata watu binafsi wako kitanzini.
Hilo limedhihirika kufuatia hivi karibuni, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kumvamia na kumfanyia upekuzi mkubwa wa saa saba, Lwitiko Adamson Mwakasala ‘Tiko’ au ‘Milionea Mtoto’  (pichani)  wakitilia shaka utajiri mkubwa alionao.

TAJ (1)-001Moja ya Nyumba anazomiliki.
ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililofunga barabara ya kutoka Sinza kwenda Magomeni lilijiri Februari 15, mwaka huu kwenye jumba lake la ghorofa lililopo Magomeni Makuti jijini Dar jirani na Kituo cha Daladala cha Kwa Bi Nyau.
TAJ (4)-001Hekalu lake jingine
UPEKUZI KWA SAA SABA
Ilikuwa asubuhi ya saa moja ambapo kikosi cha polisi kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay kilivamia kwenye nyumba ya Tiko ambayo ni ghorofa mbili ikiwa na matawi matatu na kufanya upekuzi mkubwa huku wakitaka kujua chanzo chake cha pesa mpaka kujenga jengo hilo ambalo inasemekana linaweza kuwa hoteli, shule, hospitali au ofisi.
“Upekuzi ulikuwa mkubwa sana. Tiko alianza kupekuliwa saa moja asubuhi polisi wakiwa na mjumbe wa nyumba kumi. Kazi ya upekuzi iliisha saa nane mchana,” kilisema chanzo.
TAJ (3)-001Magari yake yaliyokamatwa yakiwa kituo cha polisi
POLISI WAONDOKA NA MAGARI, WASHIKILIA GHOROFA
Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya upekuzi wao, polisi walimchukua Tiko na magari yake manane kwa ajili ya uchunguzi pia wanalishikilia ghorofa hilo huku uchunguzi zaidi  wa kujua anapataje pesa ukiendelea.
NI MATAJIRI WATATU
Ndani ya wiki moja sasa, inasemekana watu wengine wawili wenye fedha zao wamekamatwa akiwemo aliyejulikana kwa jina moja la Hemed, mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar na mwingine mkazi wa Tabata ambaye jina lake halikupatikana mara moja. Wanashikiliwa na magari yao kituoni hapo kwa uchunguzi zaidi.
WANACHOFANYA POLISI KWA SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya jeshi hilo, siku hizi polisi wanamfuata tajiri mmojammoja na kumfanyia upekuzi. Kama atakutwa na madawa ya kulevya, kesi anayo, akikutwa na mali ambazo asili yake au upatikanaje wa fedha haujulikani, pia kesi anayo.
UWAZI ENEO LA TUKIO
Kama ilivyo ada, baada ya kupata taarifa hizo, Uwazi lilifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na Mjumbe wa Shina Namba 23, Muharami Daudi ambaye alikuwepo katika zoezi la upekuzi nyumbani kwa Tiko.
“Nakumbuka ilikuwa Jumatatu, saa moja asubuhi, polisi walifika nyumbani kwangu, wakajitambulisha kuwa wametoka Kituo cha Polisi Oysterbay. Wakanitaka  nifuatane nao mpaka kwa Lwitiko katika zoezi la upekuzi wa madawa ya kulevya kwamba wana wasiwasi naye katika biashara hiyo.
“Tulikwenda kufanya upekuzi kwa pamoja, lakini hatukupata madawa ya kulevya hivyo polisi waliamua kuondoka na magari yake manane yaliyokuwa pale na bastola kwa uchunguzi zaidi,” alisema mjumbe huyo.
KAMANDA WA POLISI KINONDONI
ACP Christopher Fuime ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni. Katika mahojiano na gazeti hili, alikiri kukamatwa kwa Tiko na watu hao wengine.
“Bado tunawashikilia Lwitiko na Hemed kwa uchunguzi zaidi na kutafuta mtandao wao.
”Unajua kunahitaji uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuchunguza mali zao jinsi walivyozipata kama vile nyumba. Baadhi ya magari yao tunayo hapa tunayashikilia, tunayafanyia kazi,” alisema kamanda huyo.

No comments:

Post a Comment