Mwigizaji Kajala Masanja.
Na IMelda MteMa, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Baada ya kunasa ujauzito ambao ulisemekana ni wa kigogo mmoja serikalini, bahati haikuwa yake mwigizaji Kajala Masanja kwani mimba hiyo imechoropoka. Rafiki wa karibu na mwigizaji huyo ameliambia Risasi Jumamosi kuwa mwigizaji huyo aliugua malaria ambapo dawa alizokunywa zimemsababishia mimba hiyo ichoropoke.
“Nahisi ni madawa ya malaria aliyokunywa, huwezi amini alijisikia vibaya baada ya kumeza, ghafla akashangaa mimba imetoka,” alisema rafiki huyo wa karibu na Kajala. Ubuyu huo ulipotua kwenye dawati la Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alimtafuta mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja (Paula) ambapo alipopatikana alikiri kuwa mimba hiyo imetoka kwa bahati mbaya. “Imeniuma sana maana mwanangu alikuwa akitaka mdogo wake lakini ndiyo hivyo tena dawa zimenisababishia madhara nafikiri, mimba imetoka,” alisema Kajala.
No comments:
Post a Comment