Msanii huyo akiingia kwa sangoma.
Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan, Risasi
DAR ES SALAAM: Katika kile kinachodhaniwa kuwa ni kusafisha nyota ili mambo yake yaende vizuri, msanii wa filamu nchini, Nia Jastin hivi karibuni alinaswa akiingia kwa Sangoma mmoja maarufu ajulikanaye kwa jina la Ruta, anayefanyia shughuli zake za uganga huko Pugu Kajiungeni, jijini Dar es Salaam.

Chanzo makini kililidokeza gazeti hili kuwa kimekuwa kikimuona mara kwa mara msanii huyo akiingia na kutoka kwa sangoma huyo, kama wanavyofanya baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam wanaoamini katika ‘mambo hayo’.
“Unajua sanaa ya filamu sasa hivi imeshuka, Nia anakuja hapa kwa sangoma kila wakati. Kwa vyovyote lengo lake ni kuinua nyota yake katika filamu maana naona kama inakufa hivi,” kilisema chanzo hicho, ambacho pia ni jirani na mganga huyo.
….akijiandaa kuvua viatu.
Baada ya kupata habari hizo, mapaparazi wetu waliweka kambi kwa siku kadhaa za mwishoni mwa wiki, lakini hawakuweza kufanikiwa kumuona Nia hadi mwishoni mwa wiki iliyopita, ambavyo hata hivyo, iliwawia vigumu kumtambua kutokana na mavazi aliyovaa.
Baadaye walifanikiwa kupata picha zilizomuonesha Nia akiingia na kutoka, ingawa baada ya kuwatambua waandishi wetu aliwajia juu na kutoa vitisho kwamba endapo ataandikwa vibaya na kukataa kusema lolote.

Siku moja baadaye alipopigiwa na kuulizwa sababu ya kwenda ‘kusafisha nyota’ badala ya kupiga kazi ili mashabiki wamkubali, alikana kujihusisha na ushirikina.
“Sikwenda pale kusafisha nyota wala kufuata ushirikina, yule ustadhi mimi ni mjomba wangu, huwa naenda pale mara kwa mara ili kusomewa dua tu, kama wanavyosaidiwa watu wengine wenye matatizo yao, kama dua ni ushirikina basi sawa,” alisema msanii huyo na kukata simu.
No comments:
Post a Comment