Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Na Musa Mateja, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Mafahari wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na Omar Faraj Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ wamefika pabaya baada kutukanana mitandaoni.
Ugomvi wa wawili hao uliibuka mapema wiki hii mara baada ya Nay kuachia wimbo wake mpya redioni uitwao Shika Adabu Yako ambao amewachana mastaa wengi wa Bongo Muvi sambamba na Ommy Dimpoz aliyemwambia ana shaka kuwa ana tatizo la kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Baada ya wimbo huo kutoka na kumkasirisha Dimpoz ambaye aliibuka na kujibu mashambulizi mazito mtandaoni, chanzo kimeeleza kuwa wawili hao sasa hivi wanatafutana mtaani ili kuoneshana ubabe laivu.
Omar Faraj Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
“Yaani hii vita yao sasa imefika pabaya, watakapokutana tu wawili hawa lazima pachimbike maana kila mmoja anamuwinda mwenzake kwa wakati tofauti,” kilisema chanzo chetu.
Alipotafutwa Nay wa Mitego kuhusiana na suala hilo alisema yeye alitegemea wimbo huo utawakera wengi lakini ndiyo ukweli hivyo yupo tayari kwa lolote na yeye hana mpango wa kumsaka Ommy.
“Sina habari naye huyo kama meseji imemfikia, akae kimya,” alisema Nay.
“Sina habari naye huyo kama meseji imemfikia, akae kimya,” alisema Nay.
Demu wa ommy Dimpoz
Kwa upande wake Dimpoz naye hakutaka kukiri kuwa anamsaka Nay lakini akasema amekasirishwa sana na kitendo cha Nay kumuimba vibaya wakati kama ni mpenzi yeye anaye na anamridhisha.
“Yule wewe muache tu. Ameniboa sana. Mimi kweli niwe jogoo hapandi mtungi kweli? Aache hizo, nina demu wangu na anajua nini huwa nampatia,” alisema Dimpoz huku akimtumia mwandishi wetu picha ya mpenzi wake pasipo kumtaja jina.
No comments:
Post a Comment