Recho Ashikiliwa na Polisi Dubai

recho (2)
Winfrida Josephat ‘Recho’.
Msala! Mtoto mzuri mwenye sauti tamu kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’ anadiwa kushikiliwa na Polisi wa Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu (UAE) kwa kosa la kuzidisha muda wa kibali cha kuishi ugenini (overstay), Risasi Jumamosi lina mchapo kamili.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Recho alitoroshwa na mwanaume mwezi mmoja uliopita na kwenda kula naye bata nchini humo huku akimuahidi ahadi motomoto katika penzi lao lakini alipofika, akamtelekeza. “Alidanganywa na mwanaume, akakubali kuja naye Dubai si unajua tena mambo ya kuendekeza starehe mastaa wetu, akaja huku na alipofika jamaa akaishi naye kidogo akaingia mitini,” kilieleza chanzo chetu kilichopo Dubai na kuongeza:
HAKUMUAGA RUGE
“Kutokana na kukolea kimahaba, aliniambia hakuona hata umuhimu wa kumuaga bosi wake Ruge (Mutahaba) kitu ambacho kila mtu alimlaumu
kwani wakati huo nasikia alikuwa na project kibao za kumkuza kimuziki.”
recho (3)
MWANAUME AREJEA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa,  baadaye huyo mwanaume alimtelekeza katika nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja, alirejea na kuanza kuishi naye tena hadi pale kibali  kilipoisha na jamaa akatoweka tena wakati tayari mrembo huyo akiwa amezidisha muda wa kuishi nchini humo. Chanzo hicho kilieleza kuwa, maafande wa nchi hiyo walipombaini anaishi bila kuwa na vibali, walimkamta na kumfikisha kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano kisha wakamshikilia hadi atakapopata fedha za kulipia vibali. “Mambo huku yamemwendea vibaya, watu wameshindwa kumsaidia. Amewasiliana na ndugu,
jamaa na marafiki zake Bongo lakini imeshindikana kupata hizo fedha.
AMSAKA RUGE
“Sasa ameanza kufanya mpango wa kumtafuta Ruge ili aweze kumuokoa, maana mazingira yamemkalia vibaya kwani hana fedha hata ya nauli ya kumrejesha Tanzania na jamaa aliyemleta naye ameendelea kumpiga chenga.
recho (1)
RUGE AWATOLEA NJE
“Lakini mbaya zaidi nasikia Ruge kawatolea nje maana wakati Recho anakuja huku kumbe alitoroka hakumuaga wala uongozi wowote wa THT, alichokosea hakumuaga bosi wake huyo na tayari alikuwa ameelekezwa mambo kibao na Ruge ili aachie nyimbo mpya lakini akakaidi na kuja huku,” kilisema chanzo hicho.
RUGE HUYU HAPA
Gazeti hili baada ya kupenyezewa  mchongo huo, lilimtafuta Ruge ili kujua kama ni kweli taarifa hizo zimemfikia na kama anazo amefanya nini ili kumsaidia mrembo huyo ambaye alikuwa tishio kwa nyimbo kali ikiwemo Kizunguzungu. Ruge alikiri kuwa taarifa za mrembo huyo zimemfikia lakini bado hajafikiria cha kufanya hadi sasa.
“Nimesikia kweli anashikiliwa kutokana na mambo yake binafsi, nashindwa sana kujihusisha nayo moja kwa moja kwani hakuna jambo lolote ambalo amewahi kunihusisha kabla hajaenda huko na hata alipokuwa huku. “Bado sijaona namna ya kumsaidia maana hawa watoto nao wamekuwa  jeuri mno. Wakishajiona wamekuwa mastaa tu, hata ushauri wa maana hawapokei kabisa inanisikitisha sana,” alisema Ruge.
KUMBUKUMBU
Recho kabla ya kuondoka Bongo, alikuwa tishio kwa sauti na uchezaji wake ulioshabihiana na miondoko aliyokuwa nayo mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’. Mrembo huyo pia aliwahi kutajwa kwenye kashfa ya kutumia madawa ya kulevya lakini hakutoa majibu ya kueleweka.

No comments:

Post a Comment