Rose Muhando athibitisha kushiriki katika Tamasha la Pasaka
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, Rose Muhando amekuwa wa pili kuthibitisha kushiriki katika Tamasha la Pasaka linalotarajia mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama Muhando ameungana na mwenzake Bonny Mwaitege ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha katika tamasha hilo.
Msama alisema tamasha hilo mwaka huu linatarajia kufanyika Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28) ambako alitoa wito kutoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.
Aidha Msama alisema dhamira ya Tamasha la Pasaka ni wenye uhitaji maalum ambao ni yatima, walemavu na wajane.
Msama alisema sababu ya kupeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa ni kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo sambamba na kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’.
“Tunalipeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa kwa sababu ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo ambayo miaka iliyopita iligubikwa na mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’,” alisema Msama.
No comments:
Post a Comment