Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Stori: Mwandishi, Wetu, Ijumaa
Dar es Salaam: Aibu yake! Kitendo cha mwandani wa Mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutupia mtandaoni picha ya nusu utupu akiwa amelala na jamaa huyo, kimetafsiriwa kuwa ni kulipa kisasi kwani miezi kadhaa iliyopita naye alimtundika akiwa anaoga bafuni.
Mpenzi wa mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Picha hiyo ya mapema wiki hii, inadaiwa Zari aliitupia kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram kisha kuitoa muda mfupi bila kujua imeshachukuliwa na wapenda ubuyu na kurushwa kwenye meza ya Ijumaa.
Zari The Boss Lady akiwa na Diamond Platinumz.
DIAMOND FOFOFO
Katika picha hiyo, Zari anaonekana ndiye aliyeipiga ikiwaonesha wakiwa wamelala kitandani huku Diamond akiwa fofofo bila kujua kilichoendelea.
Picha hiyo iliibua gumzo kubwa kwa mashabiki wengi wa mastaa hao huku wengine wakidai kwamba inavyoonekana Zari aliamua kumfanyia Diamond hivyo kwani awali hakupendezwa jamaa huyo alipotupia video yake akioga.
Zari akiwa na mtoto wake.
MASHABIKI SASA
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki hao walionekana kukerwa na kitendo hicho kwani mwanamama huyo ni kioo cha jamii na kwamba nyuma yake kuna rundo la mabinti ambao wanamuiga kwa kila anachofanya.
“Zari anapaswa kutambua kwamba yeye ni role model wa wasichana wengi ambao huwa wanamfuatilia na kutamani kuwa kama yeye hivyo anachowaonesha hakiendani na matarajio yao. Kwanza yeye ni mama wa watoto wanne, anatakiwa kuachana na mambo hayo,” ilisomeka sehemu ya maoni hayo.
TEAM WEMA NDANI
Kwa upande wao, kundi maarufu linalojiita Team Wema mitandaoni, lilitumia nafasi hiyo kumshambulia kwa kumuita ‘bibi’ anayependa mambo ya wasichana wakati ni mama wa watoto wanne.
“Hivi huyu bibi anajiona bado msichana? Amesahau ana watoto wanne lakini anataka kujilinganisha na Madam ambaye usichana unamruhusu kufanya hivyo,” ilisomeka sehemu ya maoni ya mmoja wa memba wa Team Wema.
KINYUME NA MAADILI
Wengine waliandika kuwa Zari hakupaswa kutumbukiza picha hiyo ya siri mtandaoni kwani kwa mila na desturi za Kibongo siyo sawa.
“Nooo…haya siyo maadili yetu (Watanzania). Kujiheshimu ni kitu cha bure kama mama wa familia. Kwanza anawafundisha nini wanaye na familia yake? Maana unajua sasa hivi Instagram kila mtu anaona kinachofanyika,” alisema shabiki mwingine.
DIAMOND ANASEMAJE?
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili lilimsaka Diamond kwa njia mbalimbali ikiwemo kumtafuta katika WhatsApp na kumuuliza ishu hiyo lakini hakujibu.
NI TABIA YA ZARI?
Ukiacha tukio hilo, mara kadhaa Zari amekuwa akitupia picha mbovumbovu za utupu hivyo kuonekana ni hobi yake.
Mbali na yeye mwenyewe kujianika, Zari aliwahi kurekodiwa mkanda mchafu ambao ulidaiwa kusambazwa mitandaoni na aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwanga na swahiba wake, King Lawrence.
Kwa upande wake Zari amekuwa mtu wa kukaa kimya kwa maana ni mtu wa kupotezea (never mind).
No comments:
Post a Comment