Harakati za kutoa miili ya marehemu zikiendelea
Watu wanne wamefariki papo hapo na wengine 38 wakijeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kukatika viungo, kufuatia ajali ya basi iliyotokea majira ya saa tano usiku wa leo mjini Iringa.
Basi hilo lenye namba za usajili T 798 AKV mali ya kampuni ya Lupondije Express lilikuwa likitokea mjini Mwanza kuelekea mjini Iringa.
Taarifa ambazo mwandishi wa habari hizi amezipata toka eneo la tukio, zinabainisha kuwa, chanzo cha ajali hiyo, ni kufeli kwa mfumo mzima wa breki, ambapo gari hilo likiwa katika mteremko mkali wa Ipogoro, lilimshinda dereva na kugonga kingo za barabara na hatimaye kuanguka.
No comments:
Post a Comment