Dk.Kigwangalla aagiza kusimamishwa kazi kwa Wauguzi sita wa Hospitali ya Temeke kwa kuomba rushwa


Tazama MO tv, kuona video ya tukio hilo hapa: 
Wauguzi sita wa wodi ya akinamama Wajawazito wa hospitali ya rufaa ya Temeke,wamesimamishwa kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yao wakati wa kuwahudumia akina mama wanaofika kujifungua kwenye hospitali hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa kwenye ziara iliyofanywa hospitalini hapo na Naibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangwalla alipofanya ziara ya kawaida kuangalia utendaji wa kazi aliyofaya mapema leo Machi Mosi. (Machi 1.2016).
Tukio hilo la aina yake, ni mara baada ya Dk. Kigwangalla kufika Hospitalini hapo na kuangaalia huduma zinavyotolewa pamoja na kusikiliza wagonjwa, ghafla baadhi ya wagonjwa walipobaini uwepo wa Naibu Waziri huyo ndiopo walipomfuata na kutoa maoni na kero zao ikiwemo suala hilo la kudaiwa pesa za matibabu na dawa licha ya kuwa wana kadi za bima za matibabu.
Hata hivyo baada ya Dk. Kigwangalla kuhoji juu ya malalamiko yao, ndugu wa wagonjwa hao walimweleza kuwa, licha ya kuwa na Bima ya Afya, mgonjwa wao ambaye alikuwa mjamzito Wauguzi walimtaka atoe pesa ilikulipia vifaa huku wakikataa kwa kutotumika kwa kadi ya matibabu hali ambayo ni kinyume na utaratibu.
Aidha,wauguzi hao wanatakiwa kifikishwa kwenye baraza la wauguzi na wakunga kwakukosa uadilifu, waliosimamishwa kazi ni pamoja na Bi Beatrice Temba, Marian Mohamed, khadija Salum, Elizabeth Mwilawa, Agnes Mwapashe na Merion saidi.
Hatahivyo, Dk. Kigwangalla ametoa siku 30 kwa Manispaa hiyo ya Temeke kukamilisha chumba cha upasuaji cha akina mama Wajawazito. Pia ameagiza Vyumba viwili vya upasuaji kuvifanyia ukarabati mkubwa na kuwa katika ubora unaotakiwa ndani ya miezi sita.
Aidha, ametoa miezi mitatu kwa chumba cha watoto wachanga kwa kuongeza vitanda 25 hadi 30 kutoka vitanda 9 vya awali ili kuepusha magonjwa ya kuambukiza ambapo kwa sasa wodi hiyo ina vitanda tisa pekee huku wakiwa wanazalisha watoto zadi ya 30 kwa siku.
Dk.Kigwangalla ametoa wito kwa uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatekeleza yale yote aliyoagiza kwani pindi atakaporejea tena ni kuchukua hatua kwa watakaozembea.

Imeandaliwa na Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv

No comments:

Post a Comment