Gift Stanford ‘Gigy Money’.
MUUZA nyago kwenye video mbalimbali za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kwa mara ya kwanza amefungukia ishu yake ya malipo kupitia video za Bongo Fleva anazofanya kama ‘Video Queen’ kuwa kwa sasa bila shilingi milioni moja humpati.
Akichonga na Showbiz Gigy alisema kuwa, kwa sasa Muziki wa Bongo Fleva umebadilika na hata video zake zina viwango vikubwa tofauti na kipindi cha nyuma ambapo hata makampuni ya video yalikuwa machache hivyo kwa wale mastaa yupo tayari kuwafanyia kuanzia laki tano lakini kwa wale ambao hawana majina sana ‘chipukizi’ bila milioni moja hawampati.
“Kwa kawaida video nyingi huwa naanzia laki tano lakini kuna video ambazo kiukweli kabisa bila milioni moja siwezi kufanya,” alisema Gigy.
Gigy ametokelezea kwenye video kibao za Bongo Fleva ambazo ni Siachani Nawe ya Barakah Da Prince, Get High ya Godzilla, Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego na nyingine nyingi.
No comments:
Post a Comment